Psalms 34

Sifa Na Wema Wa Mungu

Zaburi ya Daudi, alipojifanya mwendawazimu mbele ya Abimeleki, ambaye alimfukuza, naye akaondoka.

1 aNitamtukuza Bwana nyakati zote,
sifa zake zitakuwa midomoni mwangu siku zote.
2 bNafsi yangu itajisifu katika Bwana,
walioonewa watasikia na wafurahi.
3 cMtukuzeni Bwana pamoja nami,
naam, na tulitukuze jina lake pamoja.

4 dNilimtafuta Bwana naye akanijibu,
akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
5 eWale wamtazamao hutiwa nuru,
nyuso zao hazifunikwi na aibu kamwe.
6 fMaskini huyu alimwita Bwana, naye akamsikia,
akamwokoa katika taabu zake zote.
7 gMalaika wa Bwana hufanya kituo
akiwazunguka wale wamchao,
naye huwaokoa.

8 hOnjeni mwone kwamba Bwana ni mwema,
heri mtu yule anayemkimbilia.
9 iMcheni Bwana enyi watakatifu wake,
kwa maana wale wamchao
hawapungukiwi na chochote.
10 jWana simba wenye nguvu
hutindikiwa na kuona njaa,
bali wale wamtafutao Bwana
hawatakosa kitu chochote kilicho chema.

11 kNjooni, watoto wangu, mnisikilize,
nitawafundisha kumcha Bwana.
12 lYeyote kati yenu anayependa uzima
na kutamani kuziona siku nyingi njema,
13 mbasi auzuie ulimi wake na mabaya,
na midomo yake kutokana na kusema uongo.
14 nAache uovu, atende mema,
aitafute amani na kuifuatilia.

15 oMacho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
na masikio yake yako makini kusikiliza kilio chao.
16 pUso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu,
ili kufuta kumbukumbu lao duniani.

17 qWenye haki hulia, naye Bwana huwasikia,
huwaokoa katika taabu zao zote.
18 r Bwana yu karibu na waliovunjika moyo,
na huwaokoa waliopondeka roho.

19 sMwenye haki ana mateso mengi,
lakini Bwana humwokoa nayo yote,
20 thuhifadhi mifupa yake yote,
hata mmoja hautavunjika.

21 uUbaya utamuua mtu mwovu,
nao adui za mwenye haki watahukumiwa.
22 v Bwana huwakomboa watumishi wake,
yeyote anayemkimbilia yeye
hatahukumiwa kamwe.
Copyright information for SwhNEN